Mtunzi: Cox Dawa Yao
Ilipoishia
Johnson alimpiga marufuku Maria kukanyaga pale Gengeni kwake Maria
akawa analia hakukubaliana na lile swala Hadi mzee Joseph jirani wa
Johnon pale Gengeni alivyoona kama hamna maelewano kati ya Johnson na
Maria akaenda kuwauliza kinachoendelea alivyoelezewa akaanza kumpa somo
Johnson
Endelea
Mzee Joseph alimwambia
Johnson mambo mengi sana yanayotokeaga kwenye mapenzi, akamshauri
Johnson asije akamuacha Maria sababu wazazi wake hawataki wawe pamoja
akamuambia waendelee na mapenzi yao tu kama kweli wanapendana ila
wafanye kwa siri sana wasijiachie ili wazazi wa Maria wasiwaletee tena
matatizo. Johnson akamwambia mzee Joseph "mzee wangu mimi
nimekuelewa na nampenda sana Maria kutoka moyoni sababu nimetoka naye
mbali sana na sijawahi kuwa na mwanamke mwengine zaidi yake hata yeye
anajua ila tatizo ndio hilo tu wazazi wake wameniambia wakija tena
kuniona naye au wakija kusikia bado nina mahusiano na binti yao
watanifunga au watanipoteza duniani na ndio maana mimi naogopa kuendelea
na Maria au kama anataka tuendelee apunguze kuja hapa Gengeni kwangu na
hata kule kwangu asije hovyo sababu tayari wazazi wake washapajua
ninapoishi wasije siku wakamkuta kule ikawa balaa"
Mzee
Joseph alimsikiliza Johnson kwa makini akamwambia "Kijana wangu mimi
nimeshakuelewa ni kweli lazima uogope sababu wazazi wake huyu binti wana
uwezo sana wanaweza wakakufanya chochote kila mimi nimekwambia we
endelea tu na mpenzi wako ila msijiachie sana kama ulisema asije sana
hapa Gengeni kwako na huko nyumbani kwako tafuteni sehemu iliyojificha
ndio muwe mnaonana huko" Johnson akamwambia yule mzee "sawa mzee
nimekusikia ahsante sana kwa ushauri wako mzuri mimi nitaendelea na
mpenzi wangu ila kuna mambo inabidi niongee naye." Muda wote huo Johnson
na mzee Joseph wanaongea Maria bado alikuwa kainama chini analia mzee
Joseph akamgeukia Maria akamwambia "We binti nyamaza usilie
nimeshamuelewesha mpenzi wako kanielewa ila kuwa makini sana usiwe
unakuja hovyo hapa Gengeni kwa Johnson utamsababishia matatizo mwenzako"
Maria aliacha kulia alifurahi sana kuona mzee Joseph kamtetea kwa
Johnson kamuelewesha hadi Johnson kakubali kuendelea kuwa naye
alimshukuru sana mzee Joseph akamwambia "ahsante sana mzee mimi nampenda
sana Johnson hata wazazi wangu wafanyaje mimi siwezi kumuacha Johnson
labda waniue" mzee Joseph alicheka sana kusikia yale maneno ya Maria
akamwambia "sawa binti hata mimi najua unampenda sababu muda mrefu sana
nawaona pamoja ndo maana nilivyoona mnalumbana hakuna maelewano nikaja
kuyamaliza" Maria na Johnson walimshukuru mzee Joseph wenyewe wakabaki
pale Gengeni wanaendelea na maongezi mzee Joseph akaendelea na shughuli
zake, Zilipita siku mbili Maria hakukanyaga gengeni kwa Johnson
wala Nyumbani kwake hadi Johnson alifurahi akaona kweli maneno ya mzee
Joseph yamefanya kazi hadi Maria kaelewa.
Siku hiyo kama
kawaida yake Johnson katoka gengeni kwake kama mida ya saa 4 usiku
akakuta pale anapowekaga funguo zake hazipo akajiuliza nani atakuwa
amechukua funguo pale na aliyekuwa anajua kuwa funguo zinawekwa pale ni
yeye na Maria.
Akausukuma mlango wake akakuta mlango wake
umefungwa kwa ndani Johnson alichanganyikiwa akawa anajiuliza nani
kaingia chumbani kwake bila ya yeye kuwepo alianza kugonga mlango kwa
nguvu akasikia sauti ya Maria ndani inamwambia "baby nakuja
kukufungulia"
0 comments:
Post a Comment