Trafiki 27 Watimuliwa Kazi kwa Rushwa

Askari 27 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani wamefukuzwa
kazi ndani ya kipindi cha miezi sita kutokana na kujihusisha na
makosa ya rushwa.Kikosi hicho ambacho kimeonya dhidi ya unyanyasaji na
ushawishi wa rushwa kwa waendesha pikipiki (bodaboda), kimesema
mikakati ya uchunguzi na upelelezi imeimarishwa kwa lengo la kudhibiti

matukio ya rushwa miongoni mwa askari wake.Akizungumza na waandishi
wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, Taifa, Mohamed Mpinga alisema askari hao wamekamatwa
kutokana na kuimarishwa kwa usimamizi wa nidhamu na mapambano dhidi
ya rushwa.Alisema, licha ya kufanya kazi kwa weledi, upo usimamizi wa
karibu kwa askari wake kwa lengo la kuepusha jeshi hilo na matukio ya
aibu yakiwemoya kujihusisha na rushwa."Pamoja na jitihada hizi
tunaomba wananchi wote kutupa ushirikiano kupambana na hali hii hasa
kwa kutoa taarifa za askari wanawaomba rushwa,"alisema Mpinga.Alisema
taarifa zitawezesha kuwashughulikia kikamilifu askari husika.Kamanda
Mpinga ameelekeza wananchi hao hususani madereva wanaoombwa rushwa na
askari, kuondokana na usiri kwa kuwafichua hata baada ya kuwapatia
fedha."Kama askari akikuomba fedha zozote ni vizuri umpatie kama
unazo. Na baada ya hapo, njoo utoe taarifa kwangu nami nitakurejeshea
fedha hizo,"alisisitiza Mpinga akisisitiza kwamba wanao wapelelezi wa
kubaini ukweli juu ya tuhuma dhidi ya askari wao.Akilenga kujibu
malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na waendesha
bodaboda dhidi ya baadhi ya askari wa usalama barabarani, Mpinga
alisisitiza,"kikubwahapa ni ushirikiano wa kila upande, utakaowezesha
tabia hii kukoma."Akizungumzia maboresho katika mifumo ya utendaji
kazi wa kikosi hicho, Mpinga alisema yamesaidia kupunguza ajali za
barabarani kuanzia Januari mwaka huu tofauti na kipindi kama hicho,
mwaka jana.Takwimu alizotoa kwa waandishi wa habari zinaonesha Januari
hadi Juni kumekuwa na ajali 2,096, vifo vinne na majeruhi 2,366
wakati mwaka jana, katika kipindi kama hicho, ajali zilikuwa11,311,
vifo 1,739 na majeruhi 9,889.Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa
na ajali nyingi ambazo ni 5,052 sawa na asilimia 60.2 ya ajali
zote.Kamanda Mpinga alisema katika utekelezaji wa kupunguza ajali
hizo, wameimarisha kitengo cha utoaji elimukwa umma na kuboresha
programu za luninga na redio kutoa uelewa kwa wananchi.Credit: Habari
leo

0 comments:

Post a Comment