Mtunzi: Cox Dawa Yao
Ilipoishia
Wazazi wa Maria walimuachia Johnson hakuamini macho yake hakutaka
tena kwenda gengeni kwake alienda kwake kupumzika huku anawaza
kutojihusisha kimapenzi na Maria tena wakati anawaza hivyo simu yake
ikaita kucheki alikuwa ni Maria
Endelea
Johnson alipata xana hasira kuona
Maria ndo anampigia simu wakati amemsababishia matatizo ile siku nzima
hajafanya kazi wala hajakaa kwa amani, hakutaka kuipokea ile simu
aliikaushia lakini Maria hakukata tamaa alizidi tu kumpigia Johnson simu
Johnson alitamani hadi aizime simu yake lakini akaona apokee asikie
Maria anamuambia nini alivyopokea tu Maria akamuuliza "vipi mpenzi wangu
mbona nakupigia simu muda wote huo hupokei" Johnson akamjibu "sikiliza
nikuambie Maria mimi sio mpenzi wako tena na kuanzia leo sitaki tena
unifuate fuate wazazi wako leo wamenipa sana tabu wameniaibisha
wamenitukana na kunitamkia maneno ya dharau sana wewe tafuta tajiri
mwenzako mimi niache sitaki kuyaweka maisha yangu hatarini kwa ajili
yako"
Maria alivyosikia vile akaanza kulia kwenye simu "Johnson mimi
na wewe tumetoka mbali sana mimi nakupenda kuliko mwanaume yoyote hapa
duniani usiwasikilize wazazi wangu hawawezi kutuachanisha mimi na wewe
na ukijaribu tu kuniacha mimi nakunywa sumu Johnson bora nife" Johnson
kusikia Maria anaongea swala la kujiua akaona bora ampe moyo sababu
akili ya Maria aliijua alikuwa akiongea kitu hatanii akajua Maria
akinywa tu sumu kwa ajili yake akafa atapata msala mkubwa sana
akamwambia "Maria najua unanipenda hata mimi nakupenda pia ila tatizo
wazazi wako hawataki wewe uwe na mimi cha kufanya sasa hivi tutulie
kwanza hadi wazazi wako wakijisahau ndo tuendelee na mapenzi yetu sababu
wanapajua hadi ninapoishi unaweza siku ukaja huku ghafla wakatokea
ikawa balaa"
Maria "baby najua unawaogopa sana wazazi wangu ila
tambua kuwa mimi siwezi kuishi bila wewe hata wazazi wangu nimewaambia
na wakiendelea kuyafuatikia mapenzi yetu mimi nitachukua maamuzi mabaya"
Yale maneno ya Maria yalimchanganya sana Johnson akampa moyo Maria hadi
akatulia lakini bado yeye msimamo wake ulikuwa ni ule ule kuachana na
Maria ili aishi mjini kwa amani
Ile siku nzima alishinda kitandani
anafikiria kile kilichomtokea kesho yake asubuhi aliwahi gengeni kwake
kama kawaida watu wote wa maeneo yale waliomuona wakati anasombwa na
wazazi wa Maria walimfuata na kumpa pole huku wengine wakimshauri
aachane na Maria asije akajitafutia matatizo. Mchana alishangaa kumuona
Maria kamfuata tena pale gengeni kwake alikasirika sana akamuambia "we
Maria mimi si nimekukataza kuja hapa baba yako na mama yako jana tu
wamekuja kunisomba hapa gengeni kwangu kwa ajili yako leo tena umekuja
hujui utanipa msala mimi"
Maria akamjibu "Sikiliza mpenzi wangu mimi
nimeshakuzoea siku ikipita bila kukuona nahisi naumwa ndo maana kila
nikitoka chuo lazima nipitie hapa gengeni kwako nikuone"Johnson mda wote
huo anaongea na Maria macho yake yalikuwa yanaangaza pande zote alikuwa
na wasiwasi wazazi wake Maria wanaweza kutokea. Johnson akamuuliza
Maria "we Maria umefuata nini hapa gengeni kwangu wakati jana tu wazazi
wako wamekuja kunisomba hapa kwa ajili yako " Maria akamjibu "Johnson
hata wazazi wangu wafanye nini mimi siwezi kukuacha wewe na siwezi
kupitisha siku bila kukuona huwa nahisi naumwa ndo maana nimekufuata
hapa Gengeni"
Akili ya Johnson ilihama kabisa alihisi muda wowote
wazazi wa Maria wanaweza kutokea pale au wakawa wameweka watu wawe
wanawachunguza kama bado wanaendelea na mapenzi yao
Johnson
akamwambia Maria "sikia Maria mimi bado akili yangu haijakaa vizuri
kutokana na mambo yaliyotokea jana wazazi wako wameniaibisha sana
wamenipotezea mda mwingi jana nimeshindwa hata kutafuta hela we nenda
tutaongea siku nyingine na sitaki unifuate hapa gengeni kwangu ukiwa na
shida na mimi nipigie simu tuongee"
Maria kusikia yale maneno
akainamisha kichwa chini akaanza kutokwa na machozi akamuambia Johnson "
Johnson we unajua kabisa mimi nakupenda sana mimi na wewe tumetoka
mbali sana simjui mwanaume mwengine zaidi yako, unazani mimi nitawezaje
kuachana na wewe kirahisi rahisi mimi ndio nimesema labda wazazi wangu
waniue ndo tutaachana mimi na wewe" Johson na Maria walibishana sana
pale mpaka wateja walikuwa wanakuja pale Gengeni na wapita njia wakawa
wanawashangaa kumuona Maria analia ila watu wengi wa maeneo yale
walikuwa wanajua Maria ni mpenzi wa Johnson sababu mara nyingi walikuwa
wanawaona pamoja. Kuna mzee mmoja anaitwa mzee Joseph ana kiduka chake
karibu na genge la Johnson alivyoona Johnson na Maria wanabishana sana
akawafwata akawaambia "Samahanini vijana kwa kuingilia maongezi yenu mda
mrefu sana naona kama mnalumbana hamuelewani hadi huyu dada muda wote
analia kuna nini jamani? Johnson akaanza kumuelezea yule mzee mambo yote
akamkumbushia hadi ile siku aliyokuja kufwatwa pale na gari akamuambia
yule mzee "Mzee Joseph unakumbuka juzi kuna gari nyeusi ilikuja hapa
kuna watu wakashuka wakanikamata wakaniambia nifunge genge wakaondoka na
mimi wale ni wazazi wa huyu binti walitaka kunipeleka polisi bahati
nzuri nikanusurika hawataki kabisa mimi niwe na mtoto wao sasa huyu
mwenzangu mimi namuambia hanielewi ndo tunachobishana hapa. Yule mzee
alimsikiliza Johnson kwa makini akamuambia "Nisikilize kijana ni kweli
unavyofanya uko sahihi lakini mwenyewe unayajua mapenzi yalivyo mtu
akikupenda anavyokua huyu binti anaonekana anakupenda kweli kutoka
moyoni cha kufanya hapa ongea naye vizuri muelewane usikubali aondoke
hapa na hasira anaweza akaenda kufanya kitu kibaya huko mwisho wa siku
upate kesi kubwa zaidi ya hiyo"
Johnson alimsikiliza mzee Joseph kwa
makini mda wote huo Maria alikuwa bado anamwaga machozi tu Johnson
akamwambia yule mzee "Sikiliza mzee mimi sina uwezo hata wazazi wangu ni
masikini sana wananitegemea mimi wazazi wake huyu binti ni maarufu sana
hapa mjini ni watu wenye pesa mimi naogopa kufungwa nisije nikapotezwa
bure"
Mzee Joseph akamuambia. Hata kama wazazi wake wana pesa
mwenzio kashakupenda hvyo hvyo na umasikini wako kwenye mapenzi lazima
kuwe na misukosuko ndo hiyo sasa unayoipata itabidi uvumilie ila tu muwe
makini hao wazazi wake wasijue kama bado mnaendelea na mapenzi yenu"
Itaendelea
0 comments:
Post a Comment