SIMULIZI: SITASAHAU NILIVYOOPOA CHANGUDOA JINI.............SEHEMU YA TANO

Mtunzi: Cox Dawa Yao

Ilipoishia
Ulifika muda braza aliondoka pale dukani akaniacha peke yangu kwa mara ya kwanza
Endelea............
Nilikaa pale dukani mda ule kulikuwa hamna wateja nikachukua magazeti nikawa najisomea mara simu yangu ikawa inaita kucheki alikuwa rafiki yangu wa karibu niliyemuacha kijijini kwetu, nilifurahi sana kuona rafiki yangu kanikumbuka nikapokea tukasalimiana.
Akaniuliza "vipi rafiki yangu unalionaje jiji la Dar es salaam?
Nikamjibu "yani rafiki yangu Dar es salaam kuzuri sana tofauti kabisa na huko ila kuna mambo ya ajabu sana kuna mambo ya kutisha sana"
Yule rafiki yangu akaguna akaniuliza "Mambo gani tena ya ajabu ya kutisha?
Nikamjibu "yani kuna warembo wazuri sana ila mambo yao yanaogopesha mchana kweupee wanavaa vinguo vya ajabu ajabu hata hawaogopi kuna sehemu moja inaitwa kimboka usiku wanajaa wadada kibao wanajiuza yani kuna mambo ya kuogopesha ambayo huko kijijini kwetu hayapo kabisa"
Yule rafiki yangu akaniambia "kumbe kweli hayo mambo yapo huko mimi nasikiaga tu hata siamini afadhali sasa hivi wewe rafiki yangu unajionea kwa macho yako wenzio huku tunalisikia tu jiji la Dar es salaam na kuliona kwenye TV na Magazeti"
Nikamuambia "sasa hivi mimi ndio niko huku japo sijatembea sana ila nishaanza kuona mambo kibao huku kuna wezi, matapeli, wakabaji, mateja yani usipokuwa makini lazima uingizwe mjini mimi braza kashaniambia kila kitu yani nipo makini sana"
Yule rafiki yangu akaniuliza "mbona mimi siwajui mateja ndio wakina nani?
Nikacheka nikamjibu "mateja ni watu wanaotumia madawa ya kulevya yani wanakuwa wameshazoea kuyatumia kila siku wakikosa pesa ya kununulia ndio wanaanza kuiba, kukaba yani sio watu wazuri kabisa"
Akaniambia "hapo nimekuelewa rafiki yangu basi kweli hilo jiji limechafuka kuwa makini sana ndugu yangu"
Niliongea na yule rafiki yangu mambo mengi sana kuna mteja mmoja wa kiume akaja nikakata simu ili kumsikiliza. Alinisalimia kwa heshima nikamuitikia vizuri tu
Akaniambia "kaka mimi nina shida na pesa kuna simu naiuza hapa"
Nikamuuliza "simu gani?"
Akanijibu "samsung Galaxy"
Nikamuambia "mimi siijui hebu naomba niione"
Yule jamaa aliingiza mkono mfukoni akatoa bahasha akaifungua akatoa simu
Nilishangaa sana kuona yule jamaa anauza simu alafu kaitoa ndani ya bahasha
Niliingalia ile simu ilikuwa nzuri sana kwa kweli niliipenda ilikuwa ya kisasa
Nikamuuliza "hii simu unaiuza bei gani?
Akanijibu "sababu nina shida na pesa wewe nipe Elfu thelasini inatosha"
Nilishangaa kuona simu nzuri kama ile inauzwa bei rahisi nikajua jamaa kweli ana shida na pesa
Sababu mimi sikuwa na pesa nikaona nimpigie braza simu nimuambie kuna simu nzuri inauzwa bei rahisi nimsikie atasemaje. Nikachukua simu yangu nikampigia braza alivyopokea tu akaniuliza "dogo vipi kuna tatizo?
Nikamjibu "hakuna tatizo kaka ila hapa dukani kuna mtu kaja anauza simu nzuri sana aina ya samsung bei rahisi sana mimi nimeipenda ndio maana nimekupigia simu kama inawezakana tuichukue"
Braza akaniuliza "hiyo simu inaitwaje amesema bei gani na anavyokuonyesha ameitoa kwenye nini?
Nikamjibu "simu inaitwa Samsung Galaxy inauzwa Elfu thelasini ameiweka ndani ya bahasha ya kaki"
Braza akaniambia "dogo achana naye huyo mti hao ndio matapeli hapo utauziwa sabuni huyo mtu kakuona wewe mgeni nimekuacha hapo dukani anataka akutapeli achana naye tena mfukuze hapo dukani"
Yule jamaa alivyoona naongea na simu muda mrefu nikaona anatoka pale dukani anaondoka zake kama kuna kitu alishtukia, mimi nikabaki nacheka tu nikajisemea kweli jiji la Dar es salaam hela zinatafutwa kwa njia nyingi. Nikasema afadhali nilimpigia braza simu ningekurupuka tu kutoa pesa za dukani kununua ile simu ingekula kwangu

Itaendelea.......................

0 comments:

Post a Comment