SIMULIZI: JOHNSON NA MARIA...........SEHEMU YA TANO

Ilipoishia
Baba yake Maria alimtolea Johnson bastola akamuambia "kijana usiposema binti yangu alipo leo nakumaliza " Johnson alibaki anatetemeka hajui afanye nini tangu azaliwe Akuwahi kuiona bastola akawa anafikiria kuwaambia wazazi wa Maria ukweli ili wamuachie
Endelea
Johnson alivyoona mambo yanazidi kuwa mazito akawa anafikiria kuwaambia wazazi wa Maria ukweli ili wamsamehe lakin pia akawa anafikiria anaweza akaongea ukweli kumbe ndio akawa amejifunga wazazi wa Maraia wakajua yeye ndio alimlaza binti yao nje ikawa balaa
Alibaki tu analia huku akiwaomba wazazi wa Maria wamuachie akawaambia yeye hajui binti yao sehemu alipo Baba yake Maria alivyoona Johnson bado hataki kusema akamwambia mke wake " Mke wangu huyu kijana mpumbavu asitupotezee muda wetu bure wakati tuna ushahidi kabisa tumevikuta baadhi ya vitu vya binti yetu huku kwake hapa cha kufanya tumpeleke kituo cha polisi tukamfungulie kesi tumuweke ndani hadi binti yetu apatikane"
Johnson alilia sana kusikia anapelekwa polisi na ile hali ya maisha aliyokuwa nayo na ndugu zake wote walikuwa hawana uwezo akajua lazima ataozea jela na pia kichwani akawa anajiuliza Maria atakuwa kaenda wapi wakati asubuhi waliachana yeye akasema anaenda nyumbani kwao.
Baba yake Maria alimkunja Johnson akamtupia ndani ya gari safari ya kwenda polisi ikaanza Johnson alikuwa analia tu anaogopa kuwaambia ukweli wazazi wa Maria
Wakati wapo njiani message ikaingia kwenye simu ya baba yake Maria aliifungua alikuwa ni housegirl wa pale kwake aliandika "Baba Maria kasharudi nyumbani msihangaike kumtafuta" yule mzee alivyosoma ile message alifurahi sana alimuonyesha mke wake ile message na yeye pia alifurahi sana. Akamuuliza mume wake "kwa hiyo mume wangu huyu mjinga tuachane naye au mimi naona anachafua gari letu tu" zile kauli zilimuuma sana Johnson ila moyoni alifurahi kusikia Maria karudi nyumbani kwao akajua ndio pona pona yake ya kupelekwa polisi.
Baba yake maria akamjibu mke wake "hapana huyu tusimuachie kwanza twende naye nyumbani tukawahoji vizuri yeye na Maria tujue kama bado wana mahusiano na pale pale tuwape onyo la mwisho wote huyu kijana amuache kabisa binti yetu"
Johnson yeye alikuwa hana tatizo na akapanga kumpotezea Maria kabisa sababu atamuharibia maisha yake atamfanya akimbie mjini

Itaendelea...........

0 comments:

Post a Comment