SIMULIZI: SITASAHAU NILIVYOOPOA CHANGUDOA JINI.............SEHEMU YA TATU

Ilipoishia                                                             
Wale wadada wakamuambia braza "Mdogo wako Handsome kama wewe tena kakuzidi hadi wewe" mimi nikacheka tu nikajua wale wadada wanataniana na braza


Braza akawaambia wale wadada "naona mmeshaanza kumtamani mdogo wangu huyu bado mdogo muacheni kabisa"
Yule mdada akajibu "huyu mbona saizi yangu kabisa yani lazima nimuibe mdogo wako nimempenda sana"
Braza akamjibu "huyu dogo hawezi kukubali kuibiwa kirahisi bado hajaanza kabisa hayo mambo naombeni mumuache mdogo wangu nimemleta hapa mjini aje kufanya kazi sio kutafuta wanawake"
Wale wadada wakacheka mmoja akajibu "hapa ndio mjini kwa jinsi mdogo wako alivyo hivyo lazima tumuibe upende usipende"
Mimi nilitulia tu nikawa nasikiliza braza anavyotaniana na wale wadada, wale wadada walikodisha Cd walizokuwa wamezifuata wakaondoka zao. Walivyoondoka tu braza akaniambia "mdogo wangu si umeona sasa wasichana wa hapa mjini walivyo resi si unaona hao wadada wameshaanza kukusifia hapo hawana lolote wanataka tu uzoeane nao waanze kukuletea mambo ya ajabu kuwa makini sana dogo hapo na wewe ukilegeza tu utachunwa mpaka mwisho"
Nikamjibu "nimewaona braza ila mimi hawaniwezi mimi nina msimamo sana wala usijali kaka yangu"
Braza akaniambia "vizuri sana mdogo wangu msimamo ndo kila kitu epuka sana vishawishi vya hapa mjini kuna wasichana wajanja sana hapa wameshakuona wewe mgeni wameshaanza kukushobokea ili wakuingize kwenye laini"
Braza aliendelea kunielekeza bei za vitu na kunifundisha mambo kibao ya pale dukani kwa vile nilikuwa nina kichwa chepesi nilijikuta ile siku ya kwanza tu nimejua mambo kibao ya pale dukani kwa braza pia alikuwa ananiambia sifa za wateja kibao waliokuwa wanakuja pale dukani ili niwajue na kuwaelewa hata kama nikiwa peke yangu wasinisumbue.
Nakumbuka kuna mzee mmoja alikuja pale dukani akawa anataka tumuwekee nyimbo kwenye memory card yake Braza akamjibu "mzee mashine yetu mbovu imezingua kajaribu sehemu nyingine"
Nilishangaa sana kuona braza kamjibu yule mzee Mashine mbovu wakati ilikuwa nzima kabisa, nilivyomuuliza kwanini kamjibu yule mzee vile braza akanijibu "dogo huyo mzee muogope sana watu wanamuita Chuma ulete hakuna mtu asiyemjua hapa yani akija dukani kwako kununua kitu ukichanganya hela yake na hela zako lazima ukute hela zako zimepungua muogope sana huyo mzee akija hapa usimuhudumie"
Nikaguna nikamuambia braza "kweli mjini kuna mambo mengi braza kila mtu anatafuta pesa kwa njia yake"
Tulikaa na braza pale dukani hadi jioni tukaanza kufunga duka tukaelekea kituoni kupanda Daladala
Sababu braza alikuwa ameshaniambia usafiri ni wakugombania nilijiweka tayari sikutaka kabisa kuzubaa
Gari ilivyokuja tu nikapanda haraka tena nikapata siti ya dirishani nilifurahi sana sababu wakati wa kuja niliinjoi sana nilivyokuwa nachungulia nje sababu nilikuwa mgeni wa jiji nilijisikia raha sana lakini Gari ilivyofika pale kwenye kona ya Buguruni sheli tuliposhukia wakati wakuja niliona mabadiliko kidogo niliona kundi la wadada wakiwa wamevaa vinguo vifupi wengine walikuwa wanavuta sigara nilishangaa sana. Nilibaki najiuliza wale wale wadada walikuwa wanafanya nini pale usiku ule wakati braza aliniambia kunakuwaga na wakabaji, vibaka, mateja nikakumbuka kuna rafiki yangu kule kijijini alinipaga stori kuwa Dar es salaam kuna sehemu nyingi sana wanawake wanafanya biashara ya kuuza mwili nikahisi hata wale wadada watakuwa wanajiuza pale ndio maana wamevaa vinguo vya ajabu lakini nikasema tukifika nyumbani lazima nimuulize braza ili niujue ukweli. Tulishuka kwenye Gari tukawa tunatembea tunaelekea nyumbani nilitamani sana kumuuliza lile swali braza wakati tupo njiani kuhusu wale wadada niliowaona Buguruni lakini nikawa naogopa. Tulifika nyumbani, tukakaa sebuleni tukaanza kupiga stori pale pale nikaingizia swali langu

Itaendelea...........

0 comments:

Post a Comment