Neymar,
alifanya Mkutano wa kwanza na Waandishi wa Habari baada ya kutoka
hospitali alipokuwa amelazwa baada ya kuumizwa mgongo katika mechi ya
Robo Fainali ya Kombe la Dunia Brazil ikiitoa Colombia.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 22 pia amesema kwamba beki wa Colombia, Juan
Zuniga amempigia simu kumuomba msamaha kwa kumpiga kwa goti mgongoni
kwenye mechi hiyo.
Hisia
kali: Neymar akibubujikwa na machozi wakati akizungumza na Waandishi wa
Habari na kusema ilibaki kidogo apooze baada ya piho la Juan Zuniga wa
Colombia
"Zuniga
alinipigia simu siku chache baadaye kuniomba msamaha na kuniambia
kwamba hakudhamiria kuniumiza," amesema Neymar. "Nimeukubali msamaha
huu, lakini siwezi kulichukulia lile kama tukio la kawaida. Siwezi hata
kusema lilikuwa tukio la makusudi, lakini kila mmoja anafahamu haikuwa kawaida. Namna alivyokuja, nyuma yangu, nisingeweza kujitetea.
"Namshukuru
Mungu kanisaidia, kwa sababu kama pigo lile lingezama ndani kwa inch
chache, ningeweza kupooza,"amesema Neymar huku akibubujikwa na machozi.
Neymar
amesema hajui mini tatizo hadi Brazil ikafungwa 7-1 katika Nusu Fainali
na Ujerumani. "Kilichotokea hakikutarajiwa. Lakini hata walipokuwa
nyuma kwa 6-0, 7-0, hawakukata tamaa, waliendelea kukimbia, kuendelea
kujaribu. Sioni ainu kuwa Mbrazil, sioni aibu kuwa sehemu ya timu hii. Ninajivunia kila mmoja katika wachezaji wenzangu,"amesema.
Anaaga: Neymar akijilazimisha kutabasamu wakati akiaga Waandishi wa Habari baada ya kumaliza Mkutano wake
0 comments:
Post a Comment